• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wahamiaji haramu 8,997 waokolewa pwani ya Libya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-10-22 19:14:30

    Jeshi la maji la Libya siku ya jumamosi limetangaza kuwa jumla ya wahamiaji haramu 8,997 wameokolewa katika pwani ya nchi hiyo katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017.

    Msemaji wa jeshi hilo bwana Ayob Qassem amesema, kwa mujibu wa data za operesheni 35 za uokoaji zilizofanywa na walinzi wa pwani na kikosi maalum cha jeshi la maji la Libya katika nusu ya kwanza cha mwaka huu, jumla ya wahamiaji haramu 455 hawakupatikana, na watu 20 kufariki.

    Machafuko yaliyozuka nchini Libya mwaka 2011 yamesababisha wahamiaji haramu wengi kuelekea pwani ya Ulaya kupitia bahari ya mediterrania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako