• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi kuu Uingereza (EPL): Manchester City yaitungua Burnley, huku Man U ikipoteza.

  (GMT+08:00) 2017-10-23 08:23:19

  Ligi kuu ya Uingereza imeendelea wikiendi iliyoisha, Manchester City ikiifunga Burnley goli 3-0. Mabao ya Man City yaliwekwa kimiani na Sergio Aguero, Nicolas Ota,endi na Leroy Sane.

  Manchester United chini ya kocha wake mwenye maneno mengi Jose Mourinho imejikuta ikiambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Huddersfield.

  Chelsea imeibuka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Watford, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Arsenal imeona mwezi baada ya kuibandika Everton goli 5-2, huku Liverpool ikichezea kichapo cha 4-1 toka kwa Tottenham Hotspur.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako