Umoja wa Ulaya umetoa euro milioni 106 kuwasaidia watu wa Sudan wanaokumbwa na maafa ya asili. Waziri mkuu wa Sudan Bw. Bakri Hassan Saleh amekutana na kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia misaada ya kibinadamu na udhibiti wa misukosuko Bw. Christos Stylianides ambaye yuko ziarani nchini Sudan kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Sudan na umoja huo kwenye misaada ya kibinadamu, kukagua miradi ya umoja huo huko Darfur na kufahamu kuhusu hali ya wakimbizi kutoka Sudan kusini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |