• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya atoa mwito wa kuwepo kwa amani kabla ya uchaguzi wa marudio

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:10:00

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliongoza maombi ya taifa, na kuwataka wakenya kudumisha amani katika upigaji kura kwenye uchaguzi wa rais wa marudio utakaofanyika Oktoba 26.

    Rais Kenyatta amewataka wakenya kutumia haki yao kidemokrasia na kujitokeza kwa wingi kupiga kura, na kutowaruhusu wanasiasa kuwagombanisha.

    Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo wakati kiongozi wa upinzani Bw Raila Odinga ametangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo, na kuwataka wananchi wasijitokeze kupiga kura, na kuwataka wajitokeze kwa wingi kwenye maandamano katika siku hiyo.

    Rais Kenyatta amesema licha ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kusema hakuna mazingira mazuri ya uchaguzi kufanyika kwa uhuru na haki, uchaguzi utaendelea kama ulivyopangwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako