• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar kuyafanyia ukarabati majumba ya kihistoria ili kuimarisha utalii

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:10:18

    Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais wa Zanzibar Bw Issa Haji Ussi, amesema serikali ya Zanzibar italifanyia ukarabati jengo kubwa na refu zaidi katika eneo la mji mkongwe Zanzibar lililoorodeshwa katika urithi wa dunia, ili kuvutia zaidi watalii.

    Bw Ussi amesema hatua hiyo inatokana na lengo la serikali kutaka kuongeza idadi ya watalii kutoka laki 4 wa sasa hadi laki 5 katika miaka mitatu ijayo.

    Jengo hilo ambalo hali yake kwa sasa sio nzuri na linahitaji ukarabati wa haraka, litajengwa kwa msaada wa fedha kutoka serikali ya Oman.

    Bw Ussi pia amesema serikali ya Zanzibar inajitahidi kuongeza idadi ya watalii kwa kuvutia wateja kutoka Russia, China na mashariki ya kati, badala ya kuendelea kutegemea zaidi soko la Ulaya na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako