• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchaguzi ya Iraq yapendekeza kufanya uchaguzi wa bunge mwezi Mei mwakani

    (GMT+08:00) 2017-10-23 09:32:15

    Tume ya uchaguzi wa Iraq imesema imewasilisha mapendekezo kwa waziri mkuu Bw Haider al-Abadi kufanya uchaguzi wa wabunge tarehe 12 mwezi Mei mwakani.

    Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Bw Jati Zubai ametoa taarifa akisema tume yake imetoa mapendekezo hayo, lakini taarifa hiyo haikuzungumzia uchaguzi wa mabunge ya mikoa, na kama jimbo la wakurdi litashiriki kwenye uchaguzi huo.

    Kwa mujibu wa katiba ya Iraq, kila awamu ya bunge inakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne. Tarehe ya uchaguzi wa bunge inatakiwa kuamuliwa na baraza la mawaziri na tume ya uchaguzi kwa pamoja, na hatimaye kupitishwa na bunge.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako