• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya watoa msaada wa fedha kwa Sudan ili kuisaidia kukabiliana na maafa ya kimaumbile

    (GMT+08:00) 2017-10-23 18:07:01

    Serikali ya Sudan jana ilitangaza kuwa, Umoja wa Ulaya umeipatia nchi hiyo euro milioni 106 ili kuisaidia kukabiliana na athari ya maafa ya kimaumbile kwa wananchi wake, na kukidhi mahitaji ya maisha ya wasudan.

    Makamu wa rais wa Sudan ambaye pia ni waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Bakri Hassan Saleh alipokutana na kamishna wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia misaada ya kibinadamu na udhibiti wa misukosuko Bw. Christos Stylianides ambaye yuko ziarani nchini Sudan, walizungumzia kuhusu maendeleo yaliyopatikana nchini Sudan katika mambo ya kibinadamu. na kisiasa.

    Bw. Christos Stylianides amesema, Umoja wa Ulaya unapenda kuimarisha ushirikiano wake na Sudan kwenye misaada ya kibinadamu, kukagua miradi ya umoja huo huko Darfur na kufahamu hali ya wakimbizi kutoka Sudan kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako