• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuanza bomoa bomoa ya nchi nzima kwa nyumba zilizojengwa kiholela

    (GMT+08:00) 2017-10-23 18:21:01

    Serikali ya Tanzania itaanza zoezi la bomoa bomoa katika nchi nzima ikilenga nyumba zilizojengwa kwenye maeneo ambayo hajapangwa.

    Akitoa tangazo hilo Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, amesema zoezi hilo linalenga kuhakikisha kuwa nyumba zinajengwa kwenye maeneo yaliyopangwa na si vinginevyo. Hatua hiyo ya serikali imekuja wakati ambapo utafiti unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya wakazi wa mjini nchini humo wanaishi kwenye nyumba zilizojengwa kiholela. Hata hivyo waziri Lukuvi amelaumu tatizo hilo kwa maofisa ambao wanafumbia macho watu wanaojenga nyumba na majengo mengine bila mpango. Amesema maofisa wengi wa mipango miji wanatumia muda wao ofisini badala ya kuwa maeneo ya ujenzi na kuahidi kupambana nao wote wanaoendelea kuzuia juhudi za serikali za urasimishaji wa ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako