• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Japan kuchukua hatua ili kuboresha uhusiano wa nchi mbili

    (GMT+08:00) 2017-10-23 19:30:13

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inatilia maanani kuendeleza uhusiano wake na Japan, na kuitaka Japan ichukue hatua halisi ili kuboresha uhusiano wa nchi hizo mbili.

    Kauli hiyo ameitoa leo hapa Beijing wakati alipozungumzia matokeo ya uchaguzi wa baraza la chini la bunge la Japan. Kutokana na matokeo ya uchaguzi huo, baadhi ya vyombo vya habari vya Japan vimeripoti kuwa Bw. Shinzo Abe ataendelea na madaraka. Bw. Geng Shuang amesema, China inaitaka Japan ifungamane na nyaraka nne za siasa na kanuni nne za maoni ya pamoja kati ya China na Japan, na kuchukua hatua ili kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati yao. Vilevile China inaitaka Japan iendelee kushikilia njia ya kujiendeleza kiamani, na kuonesha umuhimu wa kiujenzi kwa ajili ya utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako