• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tuzo ya mchezaji bora wa FIFA: Ronaldo amkalisha tena Messi

  (GMT+08:00) 2017-10-24 09:03:06

  Kwa mara ya pili Christian Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA baada ya kupata asilimia 43 ya kura zilizopigwa huku akimuacha mbali mpinzani wake Lionel Messi aliyepata asilimia 19 ya kura.

  Msimu uliopita Ronaldo alifunga magoli 12 katika Champions League huku akifunga mara mbili katika mchezo wa fainali na kuisadia timu yake ya Real Madrid kutetea kombe la Champions League.

  Zinedine Zidane yeye amewabwaga Massimiliano Allegri na Antonia Conte kwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa FIFA. Naye Gianluigi Buffon amechukua tuzo ya golikipa bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako