• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yalenga kujijenga kuwa kituo cha viwanda cha Afrika

    (GMT+08:00) 2017-10-24 09:22:40

    Ethiopia inatarajiwa kuzindua maeneo manne ya viwanda katika mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake kutimiza lengo la kujijenga kuwa kituo cha viwanda cha Afrika. Tume ya uwekezaji ya Ethiopia imesema, Kati ya maeneo hayo manne, mawili yatazinduliwa mwezi ujao katika miji ya Adama na Dire Dawa, na mengine mawili yaliyoko pembezoni mwa Addis Ababa yanatarajiwa kuzinduliwa mwezi Februari mwakani. Serikali ya Ethiopia imepanga kutumia dola bilioni moja za kimarekani kujenga maeneo 15 ya viwanda katika Kipindi cha Mpango wa pili wa maendeleo ya miaka mitano kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako