• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia ahimiza mshikamano dhidi ya kundi la Al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2017-10-24 09:53:53

    Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia ameihimiza jumuiya ya kimataifa ishikamane katika kupambana na kundi la Al-Shabaab.

    Rais Mohamed amesema hayo akitoa taarifa kuhusu ziara yake nchini Ethiopia. Pia amesema shambulizi kubwa lililotokea mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 358, limeakisi umuhimu wa mshikamano kwenye mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab.

    Ameongeza kuwa kundi hilo sio tu ni tishio kwa Somalia bali pia ni tishio kwa nchi jirani.

    Habari nyingine zinasema kamishna wa mambo ya siasa wa Umoja wa Afrika Minata Samate Cessouma ametoa wito wa kutoa fedha zaidi kwa tume ya kulinda amani wa Umoja huo nchini Somalia AMISOM, ili kusaidia juhudi za kulinda amani na utulivu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako