• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya inapanga kuwavutia wateja kwenye soko la mitaji

    (GMT+08:00) 2017-10-24 18:53:40

    Kenya inapanga kuwavutia wateja kwenye soko la mitaji kupitia uwekaji wa bidhaa zenye uvumbuzi.

    Mkuu wa Mamlaka ya masoko ya mitaji ya Kenya Bw Paul Muthaura amewaambia wanahabari mjini Nairobi kuwa, baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na risiti za akiba katika benki mbalimbali duniani, zinazowaruhusu kuuza hisa zao kirahisi kwenye soko la Kenya.

    Amesema lengo la hatua hiyo ya Kenya ni kuhakikisha mitaji zaidi inaingia nchini Kenya, na kuifanya Kenya kuwa kituo kinachoibuka cha uwekezaji. Pia amesema ongezeko la fedha zinazoingia kwenye soko la Kenya litawaonyesha wawekezaji wa kimataifa kuwa Kenya ina mazingira mazuri ya uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako