• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Madeni ya  Kenya na Tanzania yaendelea kupanda

    (GMT+08:00) 2017-10-24 19:54:04
    Madeni ya serikali za Kenya na Tanzania yameendelea kupanda na hivyo kuziweka nchi hizo mbili za Afrika Mashariki kwenye hatari ya kuwa mojawepo wa zile zenye madeni makubwa.

    Ndani ya mwaka mmoja Kenya imekopa hadi dola bilioni 7.6 kufikia Juni 2017 huku nayo Tanzania ikiwa imekopa dola bilioni 1.12.

    Deni la jumla la Tanzania la kigeni sasa limefikia dola bilioni 17 huku lile la ndani ya nchi likiwa ni dola milioni 358.

    Taakwimu za wizara ya fedha ya Kenya zinaonyesha kwamba deni la nchi hiyo limefikia dola bilioni 41.

    Mapema mwezi huu mashirika mawili ya kutathimi hali ya madeni, Moodys na Fitch, yalionya kwamba deni la Kenya huenda likafikia asilimia 60 ya pato la jumla la Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako