• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Nakumatt yafunga maduka mawili magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-24 19:55:20
    Maduka yaliokubwa na mzozo wa kifedha ya Nakumatt yamefunga matawi mawili zaidi, lile la Busia na linguini mjini Bungoma magharibi mwa Kenya.

    Mkurungezi wa maduka hayo Atul Shah hajaelezea kuhusu kufungwa kwa maduka hayo lakini amesema atatoa taarifa baadaye.

    Nakumatt imekuwa ikifunga matawi yake ambayo hayana mauzo mazuri nchini Kenya, Uganda na Tanzania.

    Wiki jana tawi lake moja katika eneo la Mlimani City mjini Dar es Salaam lilifungwa kutokana na deni kubwa la kodi ya nyumba.

    Baadhi ya matawi mengine yaliofungwa nchini Kenya ni Lunga Lunga mjini Mombasa na Nairobi matawi ya Thika Road Mall, Next Gen na Westgate.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako