• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania Serikali yafuta deni la Shilingi bilioni 76 la Kampuni ya Simu Tanzania 

    (GMT+08:00) 2017-10-24 19:55:42
    Serikali imeifutia deni la Shilingi bilioni 76 Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kuligeuza mtaji ili iweze kuimarisha uwezo na kutekeleza majukumu yake kwa ushindani.

    Kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 5(3) na 9 cha Sheria ya Fedha, Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alibadilisha deni hilo kuwa mtaji Agosti.

    Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano inasema lengo la kugeuza mkopo huo kuwa mtaji ni kuitaka TTCL kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, tija na weledi ili kuongeza ushindani katika soko.

    Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010 inazitaka kampuni zote za mawasiliano kujiorodhesha DSE. Mwisho wa kufanya hivyo ilikuwa Juni, lakini ni Vodacom pekee iliyokamilisha agizo hilo huku nyingine zikiwa bado.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako