• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zimbabwe yalaani WHO kumvua ubalozi wa heshima wa shirika hilo Rais Mugabe

  (GMT+08:00) 2017-10-24 20:39:46

  Zimbabwe imelaani hatua ya hivi karibuni ya Shirika la Afya Duniani WHO ya kumvua ubalozi wa heshima Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, na kusema kama angeambiwa mapema kuhusu kuteuliwa huko angekataa.

  Ofisa habari wa Zimbabwe Bw George Charamba amesema Rais Mugabe hakuambiwa kuhusu uteuzi wa kuwa balozi wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza barani Afrika, na mwenyewe alifahamu kupita vyombo vya habari.

  Baadaye waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe Bw Walter Mzembi aliyeongea na wanahabari akiwa na rais Mugabe mwenyewe, amesema Umoja wa Mataifa unatakiwa kufanyiwa mageuzi. Amesema hakukuwa na mawasiliano ya mdomo au maandishi kabla ya uteuzi huo, na kilichotokea kinaonyesha umuhimu wa Umoja wa Mataifa kufanyiwa mageuzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako