• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la Tanzania Daima kwa siku 90

    (GMT+08:00) 2017-10-25 09:14:15

    Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la nne kwa mwaka huu kwa kile ilichokiita uchapishaji wa taarifa zisizo sahihi.

    Mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo ya Tanzania Dk Abbas Hassan, amesema gazeti hili linafungiwa kwa muda wa siku 90 kwa kuendelea kuchapisha habari za kupotosha, ikiwa ni pamoja na habari iliyochapishwa jumapili inayosema asilimia 67 ya watanzania wanatumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI yaani ARV.

    Mwezi uliopita serikali ya Tanzania ililifungia gazeti la Raia Mwema kwa muda wa siku 90 kwa madai ya kuandika habari ya kupikwa, siku 10 baada ya kulifungia gazeti lingine la Mwanahalisi kwa muda wa miaka miwili, kwa madai kuwa lilichapisha habari ya uchochezi. Gazeti lingine la Mawio pia lilifungiwa mwanzoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako