• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchangia data zake kutoka kwenye satellite za hali ya hewa na Carbon bila malipo

    (GMT+08:00) 2017-10-25 09:21:57

    China itatoa data zake kutoka kwenye satellite zake za kisasa za Fengyun namba 4 za kuchunguza hali ya hewa, na satellite yake ya kwanza ya TanSat inayofuatilia hewa ya Carbon kwa watumiaji wa kimataifa.

    Mkurugenzi wa Kituo cha Satellite za hali ya hewa cha China Bw Yang Jun, amesema satellite hizi mbili ni matokeo ya uvumbuzi wa kisayansi na teknolojia wa China, na ni mchango uliotolewa na China kwenye kazi ya kuzuia na kupunguza madhara ya maafa.

    Pia amesema katika siku za baadaye kituo hicho kitaendelea kutoa takwimu nyingi zaidi kwa watumia katika sehemu mbalimbali duniani.

    Satellite ya TanSat ilirushwa mwaka jana, na FengYun-4 inatarajiwa kuanza kutumika mwanzoni mwa mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako