• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UM lashindwa kurefusha muda wa utaratibu wa uchunguzi kuhusu mashambulizi ya kikemikali Syria

    (GMT+08:00) 2017-10-25 09:35:48

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilishindwa kupitisha uamuzi wa kurefusha muda wa utaratibu wa uchunguzi wa pamoja kati ya Shirika la kuzuia silaha za kemikali OPCW na Umoja wa Mataifa, unaolenga kuchunguza nani alihusika na matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

    Kati ya nchi wajumbe wa baraza hilo, 11 kati walipiga kura ya ndio, wawili kura ya hapana, na wengine wawili hawakupiga kura. Russia ikiwa mjumbe wa kudumu, ilipiga kura ya hapana, kwa hivyo mswada huo haupitishwa.

    Kabla ya kupiga kura, balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa Bw. Vassily Nebenzia alisema majadiliano kuhusu kurefusha muda huo yanapaswa kufanyika baada ya ripoti ya uchunguzi kutolewa tarehe 26 Oktoba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako