• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yatuma walinzi 200 wa amani Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-10-25 09:41:24

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Meles Alem amesema Ethiopia ilituma askari 200 wa kulinda amani kwa Sudan Kusini, ili kusaidia kuimarisha amani nchini humo.

    Bw. Alen amesema askari hao wametumwa kutokana na azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu kusaidia kuimarisha amani ya Sudan Kusini.

    Mwezi Desemba mwaka jana baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 2327 kuhusu kuongeza nguvu ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ambalo limeamua kurefusha muda wa tume hiyo hadi mwishoni mwa mwaka huu, na kutoa agizo kali kwa tume hiyo kuwalinda raia wa Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako