• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapoteza dola bilioni 7 za kimarekani kutokana na hali ya sintofahamu ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2017-10-25 10:01:51

    Wawekezaji wenyeji wa Kenya wamesema, nchi hiyo imepoteza dola bilioni 7 za kimarekani katika miezi minne iliyopita kutokana na hali ya sintofahamu ya kisiasa kuhusiana na uchaguzi.

    Shirikisho la Sekta ya Binafsi la Kenya (KEPSA) limesema shughuli za kiuchumi kati ya mwezi Julai na Oktoba nchini humo zimeshuka kutokana na wasiwasi kuhusu uchaguzi.

    Wakenya walifanya uchaguzi wa rais Agosti 8, lakini Mahakama Kuu ilifuta matokeo ya uchaguzi huo Septemba 1, na kuagiza urudiwe uchaguzi mkuu ndani ya siku 60. Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo IEBC iliamua upigaji kura ufanyike alhamisi wiki hii.

    Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga anasusia upigaji kura huo kutokana na kutokuwa na mageuzi aliyoyadai kwenye IEBC.

    Ofisa wa KEPSA Bw. Patrick Obath amesema sintofahamu ya kisiasa inayoendelea inatishia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako