• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wapya wa CPC wakutana na waandishi wa habari

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:11:15

    Mkutano wa kwanza wa Kamati kuu ya 19 ya Chama cha kikomunisti cha China umefungwa leo hapa Beijing, na kumchagua Bw. Xi Jinping kuwa katibu mkuu wa kamati hiyo, kuwachagua Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji na Han Zheng kuwa wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.

    Bw. Xi Jinping amesema kutokana na juhudi za muda mrefu, ujamaa wenye umaalumu wa China umeingia kwenye zama mpya zinazohitaji hali mpya na mafanikio mapya.

    Amesema katika miaka mitano ijayo, China itakuwa kwenye kipindi cha makutano ya historia ya kutimiza malengo yake ya maendeleo, ambapo malengo ya miaka 100 ya chama na malengo ya miaka 100 ya taifa yatatimizwa.

    Pia ametoa shukurani kwa viongozi mbalimbali duniani waliotuma salamu za pongezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako