• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watengezaji bidhaa Kenya kupata hasara kutokana na hali ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:15:23
    Wenye makampuni ya utengenezaji bidhaa nchini Kenya kuwa hawatopata mapato yoyote katika muda wa miezi sita ijayo kutokana na hali ya kisiasa nchini humo.

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa jana na Chama cha Watengezaji Bidhaa nchini Kenya ambayo inasema kuwa zaidi ya asilimia 64 ya watengezaji bidhaa wamebashiri kupata hasara.

    Ripoti hiyo aidha inasema kuwa ni asilimia 2 tu ya kampuni za utengenezaji bidhaa ambayo inatarajia kupata faida.

    Hali hiyo inatokana na hali ya kisiasa inayoshuhudiwa nchini na kampeni za muda mrefu.

    Katika muda wa miezi mitatu iliyopita, ni asilimia 22 ya kampuni zilizohohojiwa zilizosema kupata mapato zaidi kwa asilimia moja na tisa ilhali ni asilimia 11 pekee zilizosema zilipokea mapato ya zaidi ya asilimia 10.

    Kulingana na asilimia 59 ya kampuni zilizohojiwa, kutoimarika kwa mapato kulitokana na kupungua kwa mahitaji ilhali asilimia 58 ya kampuni hizo zilisema kupungua kwa mapato kulitokana na sheria na sera ambazo hazina faida kwake.

    Asilimia 63 ya kampuni hizo zilisema kupungua kwa mapato kulitokana na ushindani kutoka kwa bidhaa ghushi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako