Samia alisema pamoja jitihada zinazofanywa na wadau wa benki mbalimbali kufanikisha mpango wa kuondoa maskini,bado wanawake wa ngazi ya chini hawajafikiwa kikamilifu.
Bi Suluhu aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa dunia wa wanawake na huduma za kibenki wenye kaulimbiu ya "Kuwapa fursa za kibenki wanawake".
Mkutano huo wa siku mbili ambao unafanyika jijini Dar es Salaam umevutia washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi 40 duniani na ni wa kwanza kufanyika Afrika.
Aidha Samia aliitaka Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) ambayo ilianzishwa mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kujikwamua na umaskini ,iongeze kasi ya kuwafikia wanawake ,hususan wa vijijini kwa kuongeza matawi karibu na wananchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |