• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Mwekezaji kutoka China akabidhi awamu ya kwanza ya nyumba anazojengea ufalme wa Buganda

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:16:18

    Ufalme wa Buganda jana ulikabidhiwa nyumba 42 za ghorofa na mjenzi wa China.

    Kampuni ya ujenzi ya Henan Guoji Group kutoka China ambayo ina mkataba wa ushirikiano na ufalme wa Buganda,ilikabidhi awamu ya kwanza ya nyumba 42 eneo la Kigo,wilaya ya Wakiso nchini Uganda.

    Katika makubaliano yaliyoafikiwa mwaka 2015,ufalme wa Buganda ulitoa ekari 70 za ardhi na mwekezaji alikuwa alikuwa abuni,ajenge na kufadhili ujenzi wa mtaa ambao ulipewa jina la Mirembe Villas Kigo.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa ufalme wa Buganda upande wa uwekezaji, Buganda Investment and Commercial Undertakings Limited, Bw Roland Sebuwufu, alisema awamu ya kwanza iliyokabidhiwa jana inajumuisha nyumba za vyumba vine na vitano.

    Sebuwufu amesema mradi huo utakuwa na nyumba 220 zitakazokuwa na huduma za kisasa pamoja na duka kubwa,kliniki,shule,eneo la burudani na mambo mengine ambayo yatawapatia wakazi mazingira ya kuvutia na salama.

    Mkuu wa falme ya Buganda Charles Peter Mayiga ameipongeza China na kampuni ya Henan Guoji Group kwa ushirikiano mzuri na ufalme huo akisema kwamba matunda ya ushirikiano huo yameanza kuonekana.

    Aidha aliwapongeza watu wa China kwa kuwa na maadili mema ya kazi,ambayo amewahimiza vijana walioajiriwa katika mradi huo kuiga.

    Alisema mradi huo wa nyumba sio tu utachangia kwa maendeleo ya ufalme wa Buganda lakini pia ni hatua nzuri katika kuziba pengo la uhaba wa nyumba nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako