• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalitaka baraza la usalama lidumishe mshikamano kwenye suala la silaha za kikemikali la Syria

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:34:26

    Naibu mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao jana amezitaka pande mbalimbali za Baraza la usalama zilinde mchakato wa siasa nchini Syria, na kudumisha mshikamano kwenye suala la kupambana na silaha za kikemikali nchini humo.

    Bw. Wu amesema China siku zote inapinga nchi yoyote, kundi lolote na mtu yeyote kutumia silaha za kikemikali bila kujali sababu yoyote. Ameongeza kuwa kudumisha mshikamano na kutoa sauti ya pamoja kwa Baraza la usalama, kutasaidia kupata ukweli wa shambulizi la silaha za kikemikali, na kuwakamata watu wanaowajibika, ili kuepusha kutokea mara nyingine kwa matukio ya mashambulizi ya silaha za kikemikali nchini Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako