• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Nigeria vyawaokoa watu 85 waliotekwa na kundi la Boko Haram

    (GMT+08:00) 2017-10-25 18:35:13

    Jeshi la Nigeria lisema vikosi vya serikali katika jimbo la Borno vimewaokoa watu 85 waliokuwa wanashikiliwa mateka na kundi la Boko Haram.

    Mateka hao wameokolewa jana kwenye operesheni ya pamoja, baada ya jeshi la serikali kuanzisha operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram katika maficho yao yaliyopo kwenye vijiji vinne kwenye eneo la Ngala. Vikosi vya serikali vilifanikiwa kuharibu kituo cha ugavi cha kundi la Boko Haram pamoja na karakana kwenye vijiji viwili.

    Jeshi la Nigeria limeendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki, kuwaondoa wapiganaji wa kundi hilo kwenye ngome yao katika msitu wa Sambisa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako