• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ujangili wa tembo barani Afrika unaendelea kupungua

  (GMT+08:00) 2017-10-25 18:57:46

  Shirika linalosimamia biashara ya wanyama na mimea yenye hatari ya kutoweka (CITES) limesema ujangili wa tembo barani Afrika umepungua kwa miaka mitano mfululizo, na kupungua huko kwenye nchi za Afrika kumefikia kiwango cha kabla ya mwaka 2008.

  Ripoti za idara ya shirika hilo inayofuatilia mauaji ya tembo, idara ya habari kuhusu tembo na takwimu jumuiya ya kimataifa ya ulinzi wa mazingira, zinasema hali katika eneo la Afrika Mashariki inaridhisha lakini katika eneo la Afrika ya Kati si ya kuridhisha.

  Nchini Tanzania mauaji ya tembo yamepungua kwa asilimia 55 ikilinganishwa na mwaka 2015, hii ni kutokana na hesabu ya mizoga inayopatikana. Lakini katika eneo la Afrika ya Kati mauaji hayo yamekuwa juu zaidi katika kipindi cha miaka 10.

  Nchini Tanzania kupungua huko kumetokana na walinzi wa mbuga kuwa makini zaidi kwenye utekelezaji wa sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako