• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama kuu ya Kenya yashindwa kufanya uamuzi kuhusu uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-10-25 19:21:34

    Mahakama kuu ya Kenya imeshinda kufanya uamuzi kuhusu kusimamisha uchaguzi wa rais hapo kesho au la, kutokana na idadi ya majaji kutotimia, kwa hiyo uchaguzi wa kesho utaendelea.

    Jami Mkuu Bw David Maraga amesema ni yeye tu na Jaji Isaac Lenaola, ndio walikuwepo kusikiliza kesi hiyo. Kati ya majaji saba wa mahakama kuu, kama wakiwa watano wanaweza kusikiliza shauri na kufanya uamuzi.

    Amesema Jaji Philomena Mwilu hakuweza kufika kutokana na tukio la ufyatuaji risasi dhidi ya mlinzi wake, Jaji Ibrahim Mohamed yuko nje ya nchi kwa matibabu, majaji Jackton Ojwang na Smokin Wanjala hawawezi kufika, na Njoki Ndung'u alichelewa ndege ya kurudi Nairobi.

    Kabla ya hapo shauri lilipelekwa mahakamani kuhusu kuahirisha upigaji kura, kutokana na mazingira mabaya ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako