• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika na Marekani kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya siasa kali barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-10-26 08:59:00

    Marekani na Umoja wa Afrika wamesema watashirikiana kupambana na siasa kali barani Afrika.

    Ujumbe wa Marekani kwenye Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Afrika wameanza mkutano wa siku tatu kuhusu kupambana na siasa kali kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa.

    Mshauri wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Amadou Diaw amesema bara la Afrika limesumbuliwa sana na mashambulizi kutokana na siasa kali, kubwa zaidi likiwa ni lile lililosababisha vifo vya watu 350 mjini Mogadishu.

    Naibu mkuu wa ujumbe wa Marekani kwenye umoja wa Afrika Bibi Jesica Davis Ba ameahidi kuwa Marekani itashirikiana na umoja wa Afrika kukomesha mashambulizi ya kutisha kama yale ya Mogadishu na Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako