• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa kufungua ofisi yake kusini mwa Libya

    (GMT+08:00) 2017-10-26 08:59:22

    Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mkuu wa ujumbe wa umoja huo nchini Libya Bw. Ghassan Salame, amesema ana matumaini kuwa umoja wa mataifa utafungua ofisi yake katika mji wa kusini wa Sebha ili kuimarisha mazungumzo na eneo la kusini la Libya.

    Bw Salame amesema hayo kwenye mkutano na wawakilishi wa eneo la kusini mwa Libya.

    Amewaambia wawakilishi hao kuwa msaada uliotolewa na mashirika ya kimataifa bado hautoshi, na yeye mwenyewe anajitahidi kuongeza msaada huo maradufu kwa eneo la kusini, ambako wanahitaji msaada zaidi.

    Hali ya usalama kwenye eneo hilo pia inaendelea kuwa ya utatanishi, na maofisa wa kimataifa wameshindwa kutembelea eneo hilo, ambalo linasumbuliwa na uhalifu wa uporaji wa kutumia silaha, utekaji nyara, na magendo ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako