• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yasisitiza tena ahadi ya kushiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na China

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:21:54

    Sudan imesisitiza tena ahadi yake ya kushiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na China na kufanya juhudi kutimiza malengo makuu ya pendekezo hilo.

    Kwenye kongomano la "Ushirikiano kati ya nchi za kiarabu na China na Pendekezo la Njia Hariri", msaidizi wa rais wa Sudan anayeshughulikia uhusiano kati ya Sudan na China Bw. Awad Ahmed al-Jaz, amesisitiza uhusiano imara kati ya Sudan na China, na kusema kuna nia ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana bila kuingilia mambo ya upande mwingine.

    Ameongeza kuwa Sudan imeahidi kutoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Balozi wa China nchini Sudan Bw. Li Lianhe amesisitiza tena umuhimu wa pendekezo hilo katika kuimarisha moyo wa ushirikiano wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako