• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli atarajia ushirikiano wenye ufanisi kati ya Tanzania na China kuendelea kupata mafanikio

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:22:16

    Rais John Magufuli wa Tanzania amesema, Tanzania inatilia maanani uhusiano kati yake ne China, huku akieleza matarajio makubwa kwa ushirkiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.

    Rais Magufuli amesema hayo wakati akipokea hati za utambulisho za balozi mpya wa China nchini Tanzania Bw. Wang Ke. Pia amesema, urafiki kati ya nchi hizo mbili una historia ndefu, China siku zote ni rafiki na mwenzi mkubwa wa Tanzania, na kwamba anatarajia kuwa ushirikiano wenye ufanisi kati ya nchi hizo mbili utaendelea kupata mafanikio.

    Balozi Wang amesema, China siku zote inashughulikia na kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa mtizamo wa kimkakati, na inataka kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande mbili katika sekta mbalimbali, ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako