• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, (ASFC) yazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:50:20

    Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam, (ASFC), imezinduliwa rasmi jana kwa droo maalumu kwa timu zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali. Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema michuano ya msimu huu itaanzia hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.

    Amesema kwa ujumla tu, michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, itashirikisha timu 91 msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL). Raundi ya Kwanza ya ASFC itaanza Novemba 7, 8 au 9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako