• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • David Unsworth kurithi kwa muda mikoba ya Ronald Koeman

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:50:59

    Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemthibitisha, David Unsworth kurithi kwa muda mikoba iliyoachwa na aliyekuwa meneja wa timu hiyo Ronald Koeman ambaye alitimuliwa kazi baada ya kuiongoza kwa miezi 16 ndani ya mkataba wake wa miaka mitatu. Koeman mwenye umri wa miaka 54, ameachishwa kazi siku ya Jumatatu huku akiiacha Everton ikiwa ya tatu kutoka chini ya msimamo wa ligi ya Uingereza baada ya kushinda michezo miwili pekee kati ya 13 iliyocheza.

    Uwamuzi wa kuachishwa kazi kwa Koeman umefanywa na tajiri Farhad Moshiri ambaye ni mbia mkuu ndani ya klabu hiyo na kufika kwa mwenyekiti, Bill Kenwright kisha mtendaji mkuu Robert Elstone akamuambia Koeman juu ya hatima ya kibarua chake baada ya matokeo ya 5-2 dhidi ya Arsenal.

    Beki huyo wa zamani wa kati wa Everton na timu ya taifa ya Uingereza, Unsworth mwenye umri wa miaka 44, amerithi mikoba ya Koeman akitokea timu za vijana alipochukua nafasi ya Roberto Martinez aliyetimuliwa mwaka 2016 atawasaidia vijana wa Goodison Park siku ya Jumamosi michuano ya Carabao Cup.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako