• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yaisafisha Juventus dhidi ya kashfa ya usajili wa Paul Pogba kwenda United

    (GMT+08:00) 2017-10-26 09:51:17

    Klabu ya Juventus ilikuwa ikifanyiwa uchunguzi na shirikisho la soka duniani FIFA kutokana na kile kilichodaiwa kwamba walikiuka kanuni za masuala ya usajili katika mauzo ya Paul Pogba kwenda United.

    Hiyo ilikuwa miezi michache iliyopita lakini hii jana kumetolewa taarifa mpya na FIFA ambapo shirikisho hilo la soka duniani limeisafisha Juventus katika kashfa hiyo na kusema hawakufanya kosa lolote.

    Msemaji wa FIFA katika taarifa yake amesema kamati ya nidhamu ya FIFA imefuta kesi hiyo dhidi ya Juventus na kusema kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuiendeleza kesi hiyo.

    Wakati Paul Pogba akisajiliwa na United kwa ada ya £89m mengi yalizungumzwa kuhusu usajili huo huku kiasi ambacho alikipata wakala wa Paul Pogba bwana Mino Raiola kikizua mashaka kuhusu usajili huo.

    Kwa sasa kiungo Paul Pogba yuko nje ya uwanja akiuguza majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Champions League dhidi ya Fc Basel ambapo anatarajiwa kurejea uwanjani katikati ya mwezi ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako