• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa kituo cha udhibiti wa maradhi cha China kuisaidia Madagascar kukinga na kudhibiti tauni

    (GMT+08:00) 2017-10-26 19:00:59

    Habari kutoka kituo cha udhibiti wa maradhi cha China zinasema kikundi cha wataalamu 6 kinachoongozwa na naibu katibu wa chama wa kituo hiki kitafunga safari kesho usiku kuelekea Madagascar, ambapo kinatarajiwa kufanya kazi huko kwa siku 31 ili kuisaidia nchi hiyo kukinga na kudhibiti tauni.

    Takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO zinaonesha kuwa tangu tauni izuke nchini Madagascar mwezi Agosti mwaka huu, wagonjwa zaidi ya 1,200 wameripotiwa, ambapo zaidi ya 100 wamefariki. Hatari ya maambukizi imeongezeka kwa kiasi kikubwa hivi karibuni, hivyo wizara ya afya ya Madagascar imetoa ombi rasmi ikitarajia serikali ya China kutuma kikundi cha wataalamu kuisaidia nchi hiyo kupambana na tauni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako