• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Russia atoa pongezi kwa rais Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisiti cha China

    (GMT+08:00) 2017-10-26 19:01:28

    Rais Vladmir Putin wa Russia ametoa pongezi kwa rais Xi Jinping wa China kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China. Rais Putin amesema matokeo ya uchaguzi yamethibitisha heshima ya kisiasa ya rais Xi Jinping, na kuonesha kuwa dira aliyoitoa kuhusu kuharakisha maendeleo ya uchumi na jamii ya China na kuimarisha hadhi ya kimataifa ya China imekubaliwa na watu wengi.

    Rais Putin amesema anaamini kwamba uamuzi uliotolewa kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China utasaidia kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Russia, na anatarajia kuzidi kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kusukuma mbele ushirikiano wa kiujenzi katika mambo ya kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako