Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China umepitisha marekebisho ya katiba ya chama, na kuweka mapendekezo ya kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia moja" kwenye katiba
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema marekebisho hayo yataongeza nguvu ya kuzihimiza China na nchi husika kushirikiana kujenga "Ukanda Mmoja na Njia moja", kusukuma mbele ujenzi wa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya, na kujenga Jumuia ya mustakabali wa pamoja wa binadamu.
Amesema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kutoa mchango katika kujenga dunia yenye amani, usalama, ustawi wa pamoja, usafi na mandhari nzuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |