• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa fedha wa Afrika Kusini asema nchi hiyo haimudu mpango mkubwa wa nyuklia

    (GMT+08:00) 2017-10-26 19:17:35

    Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Malusi Gigaba amesema nchi yake haiwezi kumudu mpango mkubwa wa nyuklia kutokana na ukosefu wa fedha, wakati ambao wasiwasi unazidi kuongezeka kuhusu nchi hiyo kuendeleza nishati ya nyuklia.

    Akiongea na wafanyabiashara na wanahabari mjini Cape Town waziri Gigaba amesema suala la mpango mkubwa wa nyuklia kwa sasa halitakuwepo kwa takriban miaka mitano ijayo. Kauli hiyo ameitoa kufuatia tetesi kuwa Afrika Kusini inakaribia kufikia makubaliano ya nyuklia na Russia, ambayo baadaye itaisaidia nchi hiyo kujenga kinu cha nyuklia kwa gharama ya dola bilioni 71.4 za Kimarekani.

    Hata hivyo Gigaba anatofautiana na waziri mpya wa Nishati David Mahlobo, ambaye wiki iliyopita alisema Afrika Kusini itaongeza matumizi endelevu ya nishati ya nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako