Rwanda imezishinda nchi nane za kuzalisha na kuuza kahawa zikiwemo Brazil,Colombia,Costa Rica,Ethiopia India na nyinginezo.
Jean Paul Ndamwemera meneja wa Lisa Coffee ya Rwanda amesema ushindi huo utafungua masoko mapya na kuwavutia wateja wapya.
Muungano wa wauzaji wa kahawa Rwanda umepanga kushirikiana na wakulima ili kuongeza uzalishaji na uboreshaji wa kahawa.
Rwanda ilipata dola milioni 58.5 kutoka kwa uuzaji kahawa mwaka jana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |