• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wakenya kuendelea kununua unga wa bei rahisi

    (GMT+08:00) 2017-10-26 20:11:21

    Wizara ya kilimo nchini Kenya imesema wakenya wataendelea kununua unga wa sima kwa bei rahisi ya shilingi 90 kwa kilo 2.

    Hii ni baada ya tangazo la hapo awali la kwamba kuanzia mwezi Novemba ,unga huo wa bei rahisi ulioagizwa kutoka nchi za nje utasitishwa.

    Hatua hii inajiri baada ya magunia milioni 1.1 ya unga wa mahindi kuingia nchini kutoka nchi za nje.

    Kenya ilikumbwa na ukosefu wa mahindi katika msimu uliopita na kulazimika kuagizwa mahindi kutoka nje yaliouzwa kwa bei rahisi ili mwanachi wa kawaida amudu.

    Serikali ilitumia ruzuku ya bilioni 6 kununua mahindi kwa 2300 kwa gunia kutoka shilingi elfu 4

    Hata hivyo serikali ya Kenya imepanga kuanza kununua upya mahindi ya wakulima wa Kenya ya shilingi 3400 kwa gunia baada ya mahindi ya nje kumalizika katika maghala ya kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako