• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kutumia utalii kuhimiza ongezeko la uchumi

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:08:40

    Afrika ya Kusini kwa sasa inatekeleza mipango mbalimbali ya kuhimiza sekta ya utalii, na kutumia mipango hiyo kuhimiza ongezeko la uchumi, nafasi za ajira na kupambana na umaskini.

    Ofisa mkuu wa bodi ya utalii ya Afrika Kusini Bw Sisa Ntshona amesema bodi hiyo imeanza kutekeleza mpango wa 5 kwa 5, wenye lengo la kuvutia watalii milioni 5 zaidi.

    Mpango wa 5 kwa 5 ni mkakati mpya wenye lengo la kuvutia watalii milioni 4 kutoka nchi za nje, na wengine milioni 1 wa ndani. Pia unawahimiza watu wa Afrika Kusini kufanya utalii wa ndani. Wenyeji wa nchi hiyo wamehimizwa kufanya safari za ndani za utalii na kujionea vivutio mbalimbali vya nchi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako