• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchaguzi ya Kenya yaahirisha upigaji kura kwenye kaunti zilizokumbwa na vurugu

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:09:03

    Tume ya uchaguzi ya Kenya imesema upigaji kura kwenye kaunti nne za magharibi ulikwamishwa na maandamano yenye vurugu, na upigaji kura kwenye kaunti hizo utafanyika kesho.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Ezra Chiloba amesema uchaguzi umeahirishwa katika kaunti za Homabay, Siaya, Migori na Kisumu, maeneo ambayo ni ngome kuu ya upinzani. Sababu kubwa ni vurugu na vitisho dhidi ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi.

    Hata hivyo wapinzani wamesema wanashangazwa na kusogezwa mbele kwa upigaji kura katika kaunti hizo nne, na kusema upigaji kura pia haukufanyika katika maeneo ya kaskazini, mashariki na pwani. Uamuzi huo umeonekana kama ni ukabila.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako