• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa atoa mwongozo wa kutatua suala la Yemen

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:33:45

    Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Cheikh Ahmed ametoa mwongozo wa kutatua suala la Yemen, unaolenga kujenga uaminifu na kukomesha makabiliano kati ya pande mbalimbali.

    Bw. Ahmed amesema juhudi zinafanyika ili kutafuta ufumbuzi wenye ufanisi wa suala la Yemen. Amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaweka kipaumbele katika kuhakikisha pande mbalimbali zinatunga upya azimio la kusimamisha mapambano, kujenga uaminifu, na kuzirejesha pande husika kwenye meza ya mazungumzo, ili kutimiza makubaliano ya amani ya pande zote.

    Wakati huohuo, Bw. Ahmed amezitaka pande mbalimbali zilegeze misimamo yao ili kuweka msingi wa kutimiza amani ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako