• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia waongea kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:42:20

    Rais Xi Jinping wa China jana aliongea kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin wa Russia. Kwenye maongezi yao rais Putin amepongeza kufungwa kwa mafanikio kwa Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kumpongeza Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa chama. Amesema fikra ya ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya iliyotolewa kwenye mkutano huo, ina umuhimu mkubwa. Pia amesema anapenda kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kudumisha mawasiliano ya karibu na rais Xi kuhusu masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda.

    Kwa upande wake Rais Xi Jinping ameshukuru salamu za pongezi za rais Putin, akieleza kuwa mkutano mkuu wa 19 wa CPC umeweka mwongozo na mipango ya utekelezaji kuhusu maendeleo ya chama na nchi katika siku za baadaye.

    Pia amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Russia kukuza uhusiano kati ya pande hizo mbili na kupata mafanikio zaidi ili kuwanufaisha watu wa pande hizo mbili na nchi nyingine duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako