• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping atoa agizo la kujenga jeshi lenye nguvu

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:42:57

    Katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Xi Jinping amesema, jeshi la China linapaswa kuchukua hatua thabiti kujengwa kwa jeshi lenye nguvu, wakati ujamaa wenye umaalumu wa China unapoingia katika zama mpya.

    Bw. Xi amesema hayo alipokutana na maofisa waandamizi wa jeshi mjini Beijing.

    Katibu mkuu Xi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya Kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China anataka jeshi lijifunze na kutekeleza kwa makini kanuni za mkutano mkuu wa 19 wa CPC, kufuata njia ya kulijenga kuwa jeshi lenye nguvu likiwa na umaalumu wa China, na kusukuma mbele mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa ya ulinzi na ya kijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako