• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Timu zitakazokwaana robo fainali Carbao Cup zapatikana

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:49:22

    Michuano ya Carbao Cup iliendelea juzi ikishuhudiwa vigogo wakubwa wa Epl Manchester City, Manchechester United na Arsenal wakifanikiwa kufuzu kwa ajili ya robo fainali.

    Jana kulikuwa na droo ya kupanga mecho za robo fainali, katika upangaji huo wa robo fainali haitashuhudiwa mechi baina ya vigogo wa ligi katika robo fainali kwani hakuna mchezo wanaokutana katika hatua hiyo.

    Chelsea ambao wameitoa Everton juzi sasa watakutana na Afc Bournamouth katika robo fainali huku West Ham ambao waliitoa Tottenham Hotspur watakabiliana na Arsenal katika. Mabingwa wa msimu wa juzi Leicester City watakutana na vinara wa ligi kuu ya Epl kwa sasa Manchester City huku majirani wa City klabu ya Manchester United watakuwa wageni wa Bristol City.

    Robo fainali ya Carbao Cup inatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 19 na 20 ya mwezi wa 12, na hiyo itatoa timu zitakazokwenda kucheza nusu fainali ya michezo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako