• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La Liga na Copa del Rey kuanza kutumia teknolojia ya VAR viwanjani

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:50:48

    Bosi wa shirikisho la soka nchini Hispania RFEF, Juan Luis Larrea amesema teknolojia ya Video Assistant Refaree (VAR) itaanza kutumika kwenye La Liga na Copa del Rey kuanzia msimu ujao. Ligi kuu ya Hispania ni moja ya ligi tano bora barani Ulaya ambazo hazitumii teknolojia ya usaidizi wa video, (VAR) ambayo itatumika rasmi kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi. Kwa upande wa Rais wa LaLiga, Javier Tebas amesema kuwa teknolojia hiyo ni ghali sana, lakini Larrea amesema RFEF ipo tayari kukubali mabadiliko hayo bila kujali gharama zake. Aidha Larrea amesisitiza kuwa kuna teknolojia zinakuja kwenye soka na inapaswa kuzibali kwasababu zinasaidia kuondoa utata kwenye mchezo pendwa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako